Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu
ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada
ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa
imekataa kuzungumzia udaku
wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu
kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50,
aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu
hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo
imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa
mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa
kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku
nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne
pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba
kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi
Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu
kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi
cha takriban miaka ishirini.

Chapisha Maoni