Dodoma.
Wakati mjadala kuhusu sura ya kwanza na sita kwenye Bunge Maalumu ukielekea
ukingoni, baadhi ya wajumbe wametoleana kauli ambazo zimesababisha kutoelewana.
Kiini
cha hayo ni aina ya muundo wa Muungano unaotakiwa kuwekwa kwenye Katiba Mpya,
suala ambalo wajumbe badala ya kulijadili kwa hoja, wakaishia kushambuliana kwa
maneno.
Kwa
muda mrefu hali haikuwa shwari, kwani dakika 10 zilizotengwa kwa ajili ya
mjumbe kuchangia mjadala, wengi walizitumia kumaliza hasira dhidi ya wenzao au
kuponda
mchango uliotolewa awali na mjumbe mwingine.
Hebu
tuone mifano ya kauli zilizoacha majeraha bungeni hivi karibuni.
Kauli
ya Lukuvi
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema
Chama cha Wananchi (CUF) ni sehemu ya kikundi cha Uamsho kinachoisumbua
Serikali ya Zanzibar.
Lukuvi
akaenda mbali zaidi na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif
Sharifu Hamad, ni mchochezi ambaye amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvuruga
Muungano na kudai anastahili kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya
Jinai The Hague - Uholanzi.
Kauli
hii inaweza kuonekana kama njia ya kuzuia wananchi wasikiamini Chama cha CUF
katika mchakato wa Katiba Mpya.
Profesa
Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti
wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihitimisha hotuba kwa mujibu wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), akalifananisha Bunge Maalumu na kundi la
Intarahamwe.
Kundi
hilo ni lile lililoendesha mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994.
Felix
Mkosamali
Mbunge
wa Muhambwe, Felix Mkosamali alisema Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, ni viongozi vigeugeu ambao hawawezi
kufikisha nchi mahali popote.
Kiumri
Mkosamali ni mdogo kuliko wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Alisema
nchi haiwezi kuendelea kuongozwa na viongozi vigeugeu, kauli ambayo
imewachukiza zaidi viongozi wa Serikali.
Vijembe
kutoka Zanzibar
Mwakilishi
wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa alieleza kuwa baadhi ya wajumbe wenzake kutoka
Zanzibar ‘wameufyata’, akimaanisha hawakutetea walichokubaliana kabla ya kufika
Dodoma.
Hata
hivyo, naye akapigwa kombora na Asha Bakari Makame, ambaye alitafsiri kuufyata
kuwa ni sawa na mtu mwenye busha.
Akaeleza
bungeni kuwa mwenendo wa maisha ya Jussa unatia shaka kwa sababu ana umri
mkubwa, lakini hajaoa wala hana watoto.
Masauni
na Kupindua Serikali
Hamad
Masauni Yussuf alituhumu wanaopinga Serikali mbili kuwa ndiyo wamekuwa na mbio
za kutaka kupindua Serikali.
Pia
alisema kauli za wajumbe hao zinaifafanisha hati ya Muungano na barua ya
mapenzi, akaeleza bungeni kuwa watakaporejea Zanzibar watawahangaikia watu hao
hata kama watajificha shimoni.
Omary
Ali Shehe
Huyu
naye akaibuka na kauli tata akisema, “Wanaolazimisha serikali mbili mpaka
kutokwa povu mdomoni ni wanafiki na wasaka tonge.”
Mrema
na Sanya
Mbunge
wa Vunjo, Augustino Mrema alishauri watu wasikubaliane na Serikali tatu kwa
sababu hali ya usalama ya taifa siyo shwari, hasa kwa Zanzibar aliyodai
inanyemelewa.
Mohammad
Sanya
Mkongwe
huyu wa siasa za upinzani Zanzibar akaita wawekezaji kutoka Tanzania Bara
waliopo visiwani humo kuwa ni wauza karanga na dawa za mende. Alitaka Zanzibar
iachwe ijijenge kwa kiwango cha kuwa Dubai na Hong Kong nyingine.
Diana
Chilolo
Anasema
ana shaka juu ya Tundu Lissu kufunga ndoa na wajumbe kutoka Zanzibar na kwamba
anashangaa ndoa hiyo ni ya aina gani.
Lissu
na Askofu
Tundu
Lissu alisema kukosoa yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, siyo
dhambi kwa kuwa hakuwa Malaika wala Mungu hivyo alipokosea lazima akosolewe
hadharani.
Chapisha Maoni