Waziri mkuu nchini Korea Kusini
amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry
iliozama siku kumi na moja zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa
kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomwa
alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika
ferry hiyo ya
Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa
maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani
waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara
ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea
kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu
wote wametolewa katika boti hiyo.

Chapisha Maoni