Marekani imetoa taarifa kuhusu
vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi na kuushutumu utawala wa Moscow kwa
kushindwa kutimiza mkataba wa kimataifa uliolenga kusuluhisha mzozo wa Ukraine.
Vikwazo hivyo vimelenga washirika
wa Karibu wa Rais wa Urusi Vladmir Putin na vimeongeza orodha ya vikwazo
vilivyowekwa hapo awali kwa baadhi ya maafisa wa nchi hiyo baada
ya Moscow
kutwaa eneo la Crimea mwezi uliopita.
Miongoni mwa waliolengwa ni mmoja
wa wanasiasa maarufu nchini Urusi Igor Sechinambaye wakati mmoja alikuwa afisa
wa ujasusi na sasa ni afisa mkuu katika kampuni ya mafuta ya Rosneft ambayo kwa
kiwango kikubwa inadhibitiwa na serikali.
Karibu asilimia sitini ya kampuni
hiyo inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya uingeza BP na thamani ya hisa za
kampuni hiyo ilishuka punde tu baada ya taarifa kuhusu vikwazo hivyo kutolewa.
Wengine waliolengwa ni Alexei
Pushkov, ambaye huongoza kamati ya mambo ya nje katika bunge la Urusi,Naibu
waziri mkuu na kampuni kumi na saba za Urusi.
Akizungumza hapo awali Rais Putin
alisisitiza kuwa Ukraine haitaathirika kiuchumi kutokana na vikwazo hivyo.
Rais wa Marekani Barack Obama
amesema nia ya Marekani sio kumlenga moja kwa Rais Putin lakini ni katika
juhudi za kuishawishi Urusi kufuata mwelekeo unaofaa.
Muungano wa Ulaya pia umetangaza
vikwazo vya usafiri na kuzuiliwa kwa mali dhidi ya watu 15 nchini Urusi lakini
majina yao bado hayajatajwa.

Chapisha Maoni