Makamu wa Rais wa Marekani Joe
Biden amesema sharti Urusi ikome kuongea sana na badala yake ianze kufanya kazi
ya kusitisha mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine.
Bwana Biden aliyasema hayo wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ambapo waziri mkuu wa Ukraine
Arseniy
Yatsenyuk pia alihudhuria.
Marekani imeonya Urusi kuwa
ikiendelea kuchochea hali nchini Ukraine , itatengwa na jamii ya kimataifa. Pia
ameitaka Urusi kukomesha uungaji mkono wa vikosi vya Ukraine vinavyounga mkono
Urusi.
Joe Biden, amesema kuwa Marekani
iko tayari kuwasaidia viongozi wa Ukraine kufikia kile alichokitaja kuwa fursa
ya kihistoria ya kujenga taifa la Ukraine lenye umoja.
Biden pia aliwahutubia wabunge
mjini Kiev katika ziara iliyopangwa kuonyesha uungwaji mkono wa Marekani kwa
serikali ya mpito ya Ukraine.
Bwana Biden amesema kuwa uchaguzi
wa urais uliopangwa kufanyika mwezi ujao ni muhimu zaidi katika historia ya
taifa hilo.
Wakati huohuo Biden amesema kuwa
Marekani haitawai kutambua alichosema ni Udhibiti haramu wa jimbo la Crimea
ambalo linadhibitiwa na Urusi.
Amesisitiza kuwa Ukraine ni nchi
moja na inapaswa kusalia hivyo.
Amesihi Urusi,kuhakikisha kuwa
mkataba uliofikiwa wiki jana wa kusitisha mgogoro kwa kuamuru vikosi vya
Ukraine vinayounga mkono Urusi nchini humo kuondoka katika majengo ya serikali
waliyoyateka Mashariki mwa Ukraine.
Kadhalika Biden alisema kuwa
pamoja na msaada zaidi wa dola bilioni 50 unaodhamiria kusaidia kuchepua uchumi
na kuleta mageuzi ya kisiasa,Marekani pia inaahidi kutoa msaada wa kijeshi.

Chapisha Maoni