Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
amekuwa akiongoza sherehe za kutimiza miaka 20 ya demokrasi na kumalizika kwa
utawala wa ubaguzi wa rangi.
Akihutubia taifa Rais Zuma
alisema Afrika Kusini inaanza kupona vidonda vya historia ya ukatili na
mgawanyiko na taratibu inajenga umoja wa taifa.
Lakini alisema bado kuna kazi ya
kukamilisha lengo la kuondosha umaskini, tofauti za pato na ukosefu wa ajira.
Sherehe hizo zinafanywa kabla ya
uchaguzi mkuu ambapo chama tawala cha ANC kinakabili upinzani dhidi ya uongozi
wa nchi tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka wa 1994.

Chapisha Maoni