Waziri mkuu nchini Mali Oumar
Tatamy Ly pamoja na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu,miezi minane tu baada
ya demokrasia kurudi nchini humo kufuatia udhibiti wa eneo la kazkazini
uliotekelezwa na wanamgambo wa kiislamu.
Mabadiliko katika serikali yalitarajiwa kufanyika
,lakini taarifa katika mji mkuu wa Mali Bamako,zinasema kuwa kiwango cha mabadiliko hayo hakikutarajiwa.
Waziri mkuu mpya ,Moussa Mara amekuwa mpinzani mkuu wa rais Boubakr Keita hapo awali.
Bwana Mara aliye na umri wa miaka 39 amekuwa akiitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la kazkazini la nchi hiyo.

Chapisha Maoni