Kumezuka mapigano kati ya jeshi la polisi na
wakaazi wenye hasira usiku kucha katika mojawapo ya viunga vya mji wa Rio de
Janeiro
Barabara zimefungwa mjini humo
wakati risasi zikisikika kutoka eneo hilo na polisi iking'ang'ana kuwadhibiti
wakaazi
hao.
Picha zinazoonyeshwa moja kwa
moja kwenye runinga zinazochukuliwa kupitia kwenye helikopta zimethibitisha
wazi kuwa barabara kuu muhimu katika mji mkuu wa rio zinazopakana na ufuo wa
Bahari zimefungwa na polisi wa trafiki wanaojaribu kutuliza ghasia hizo.
Wakati mmoja; mwandamanaji
alionekana na bunduki na magari yanayonekana yakiteketea kando ya barabara
ambazo awali zilikuwa gizani kwa sababu ya kutoweka kwa umeme.
Ghasia hizo zilianza kufuatia
kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 26, ajulikanaye kama Douglas Rafael da
Silva, mchezaji densi wa kulipwa. Kulingana na familia yake mwili wake
ulipatikana ukiwa umejaa vidonda na waliwalaumu maafisa wa polisi kwa kumpiga
hadi kufa baada ya kumshuku kuwa mwanachama wa genge moja linalouza madawa ya
kulevya.
Makundi makubwa ya watu
yalikusanyika katika lango la kuingia katika makaazi hayo ya mabanda
alikopatikana mtu huyo ameauwa na wakataka kujua kutoka kwa maafisa wa polisi
sababu za kuuliwa kwake. Polisi kadhaa wa kijeshi wenye silaha wako mahali hapo
kufuatia habari kuwa kituo cha polisi kilichoko mahali hapo kimevamiwa.
Pavaozinho ni mojawapo ya makaazi
ya mabanda ambayo Serikali Kuu ya Brazil imejaribu kuwatimua magenge ya
walangunzi wa madawa ya kulevya wenye silaha kutoka kwa jamii na kueneza amani
na mmalaka ya polisi.
Polisi wamekiri katika mahojiano
na BBC kuwa wameshindwa kuthibiti usalama katika makaazi ya mabanda katika mji
mkuu wa Rio de Jenairo, muda mfupi tu wakati ambapo wageni wengi wanatarajiwa
nchini humo, kukiwemo maelfu wanaotarajiwa nchini kwa sababu ya Kombe la Dunia.
Wakati huohuo maafisa wa polisi
nchini wamealumiwa kwa kupendelea kutumia nguvu katika kutuliza ghasia
zinazoendelea nchini.

Chapisha Maoni