Umati mkubwa wa watu
wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi
wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa John XXIII
wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja
kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict
XVI imeangaliwa na karibu
mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya
televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100
wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na
serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa
wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema
hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda
mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.
Taarifa zinazohusiana

Chapisha Maoni