Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri iliyotolewa na Rais kupitia
kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika
wadhifa wake mara moja.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na
vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji
ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa
ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa serikali kwa
kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu
punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan
Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi
waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia
katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka mji wa
Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa wametafuta
hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata hivyo waasi wanaomuunga
mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN kuwa
walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio
katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.

Chapisha Maoni