BARAZA la Vijana wa CHADEMA
(Bavicha) limemtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kulalamika kuhusu dawa za
kulevya zinazopitishwa kwenye viwanja vya ndege kwa kuwa ameshindwa
kushughulikia majina ya wafanyabiashara hiyo aliyowahi kukiri kuwa nayo.
Alisema Bavicha imefedheheshwa na
kauli hiyo ya mkuu wa nchi, kwa kuwa haina mashiko wala haisaidii katika
kupambana na biashara hiyo haramu.
“Bavicha inaona kauli hii ya Rais
Kikwete ni dhihaka kwa vijana wa taifa hili ambao ndio waathirika wakubwa wa
dawa za kulevya kwani haina dhamira pana ya kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo.
“Ikumbukwe kuwa tangu rais atamke
kuwa anayo orodha ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya hakuna hatua zozote
alizochukua dhidi ya watu hao, zaidi taifa limeendelea kuathirika na biashara
hiyo haramu.
“Bavicha inajiuliza kulikoni mkuu
wa nchi anaayakumbatia majina ya wanaoliangamiza taifa bila kuchukua hatua
zozote? Je, anawaogopa? Ama ni maswahiba zake kiasi cha kuona aibu kuwachukulia
hatua?
Kutokana na hali hiyo, Bavicha
inamkumbusha Rais Kikwete kwamba, inachafua taswira yake kama kiongozi wa nchi
pia kushusha hadhi ya Ikulu kwa kuwa inaonekana ni kituo cha kuhifadhi
wahalifu.
Alisisitiza kuwa Bavicha inamtaka
Rais Kikwete kutambua kuwa maneno bila matendo katika kupambana na dawa za
kulevya nchini hakusaidii bali kunaendelea kupalilia uharamia huu, hivyo
imefika wakati wa kuwataja hadharani wale wote anaowafahamu
wanaojihusisha na biashara hii kisha awachukulie hatua.
Juzi Rais Kikwete alinukuliwa
akisema kwamba haridhishwi na kasi ya kupambana na dawa za kulevya katika
viwanja vya ndege hapa nchini.

Chapisha Maoni