Home » » G7 yazidi kuibana zaidi Urusi

G7 yazidi kuibana zaidi Urusi

Written By Unknown on Jumamosi, 26 Aprili 2014 | 14:25

Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa viwanda duniani G7 wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema wataanza kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya
jumatatu na wanatarajia
kulenga biashara za binafsi na ambazo zina uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.

Viongozi hao wa G7 wameelezea kuguswa kwa na jinsi Urusi ilivyoshindwa kuacha kuwasaidia wanaoipinga serikali.
Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. bentabless.com - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger