Home » » bungeni maoni binafsi ya kamati no.1

bungeni maoni binafsi ya kamati no.1

Written By Unknown on Jumamosi, 12 Aprili 2014 | 09:40

Dodoma. Zogo kubwa limezuka Bunge Maalum la Katiba wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kamati baada ya mmoja wa wenyeviti wa kamati hizo kudaiwa kukiuka kanuni.
Mwenyekiti wa Kamati Na. 1, Ummy Mwalimu, ametuhumiwa kukiuka kanuni kutokana na kutokusoma ripoti iliyoainisha maoni ya timu yake kama ilivyoandikwa.
Wajumbe walidai kuwa Mh. Mwalimu
ametoa maoni yake binafsi ambayo hayapo kwenye taarifa ya kamati.
Pamoja na jitihada za Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, kupoza rabsha hizo, Mh. Mwalimu alizidi kuzua zogo pale aliporuka baadhi ya mapendekezo ya Walio Wachache katika ripoti yake.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. bentabless.com - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger