ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, amewapongeza wajumbe wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuondoka bungeni huku akisema wajumbe walibaki
wanaendesha ‘bunge la mzaha’.
Akizungumza na Tanzania Daima
jana alisema wabunge wa waliobaki wamekuwa wakijadili mambo yasiyo ya maana
huku wakiendelea kula kodi za wananchi.
Mwamalanga alisema ni jambo la
ajabu na kushangaza kwa mjumbe kutumia Biblia kuwatukana wajumbe waliotoka.
“Bunge linaloendelea sasa
ninaliita ni bunge la mzaha na kwamba wananchi wakae chonjo hawatapata chochote
kutoka humo, wanachofanya sasa ni kuendelea kula fedha za wananchi kupitia kodi
zao,” alisema Mwamalanga.
Alisema CCM imepoteza sifa
kutokana na wanachoendelea kufanya bungeni na kwamba hata baadhi ya
viongozi wa dini wamewahama kutokana na kejeli wanazozifanya.
Pia aliwashangaa wajumbe
wanaoidharau Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofanya kazi ya kukusanya mawazo
ya wananchi huku akisema dawa iliyopo ni kuwepo kwa serikali ya shirikisho.
Chapisha Maoni